• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mdau atoa vifaa kujikinga na Corona Kondoa

Tarehe iliyowekwa: May 14th, 2020

Mmiliki wa mabasi ya Machame William Lucas ametoa sabuni na vitakasa mikono kwa ajili ya kuwasaidia watu waliokatika hatari zaidi ya kuambukizwa virusi vya Corona katika Wilaya ya Kondoa na Chemba.

Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wawakilishi wa vituo vya kulelea watoto yatima na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa  Mhe. Sezaria Makota amemshukuru mdau huyo na kumuahidi kuwa vifaa hivyo vitafikishwa kwa walengwa waliokusudiwa na si vinginevyo na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa mdau huyo.

“Bwana Lucas ameguswa sana jinsi Serikali inavyopambana na janga hili la Corona, na ameona ni vyema kushiriki katika mapambano hayo ambapo ametoa chupa 800 za sabuni ya maji pamoja na chupa 720 za vitakasa mikono, msaada huu utakwenda moja kwa moja kwa walengwa ambao ni vituo  viwili vya kulelea watoto yatima, Polisi na Magereza pamoja na Vituo vyote vya Afya na Hospitali “.Alisisitiza Mhe. Makota.

Hata hivyo aliongeza kuwa pamoja na kutoa msaada huo katika ukaguzi wa mabasi uliofanya na Kmati ya Ulinzi na usalama mabasi ya kampuni ya Machame yapo mstari wa mbele kwa kuhakikisha taratibu zote za kupambana na maambukizi ya virusi ya Corona zinafuatwa na kuwasihi wamiliki wengine  kuendelea kuchukua tahadhali zinazotolewa na wataalamu wa afya jinsi ya kujikinga na corona kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kila mara.

Akiongea katika hafla hiyo Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Machame Bwana William Lucas amesema kuwa anategemea kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wengine ili kwa pamoja waunganishe nguvu zao katika kuendelea kupambana na janga hilo la Corona ambalo limekuwa kikwazo kikubwa katika ukuaji wa  uchumi na maendeleo kwa ujumla.

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa Bwana  Nicholaus Kasendamila  amesema kuwa msaada huo ni msaada mkubwa na muhimu kwani umeisaidia Serikali kupambana kudhibiti hali ya Corona nchini na kumuomba bwana Lucas kuwa balozi wa kuhamasisha wengine kujitoa na kusisitiza kuendelea kuwa pamoja katika kukabiliana na janga hili kwa pamoja. 

Hata hivyo mmoja wa wanufaika wa msaada huo ambaye ni mlezi msaidizi wa kituo cha Poloni Mission Sista Monica Irine amemshukuru mdau huo kwa upendo na moyo wa imani wa kuamini kuwasaidia wasiojiweza bila malipo yoyote na anaimani Mwenyezi Mungu atambariki kwa jambo hilo.

Mkuu wa Wilaya amepokea vifaa vya kujikinga na Corona kutoka kwa mdau huyo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa harakati za kupambana na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona  ambapo hafla hiyo ilihudhuliwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali, waandishi wa habari pamoja na wananchi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa