• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Ustawi wa Jamii
    • Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RC Senyamule aongoza Wanawake wa Dodoma kuadhimisha siku yao Duniani

Tarehe iliyowekwa: March 8th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Mhe. Rosemary Senyamule ameongoza viongozi wa Kiserikali, Chama, Vyombo vya Ulinzi na Usalam, Taasisi , Mashirika, Dini Pamoja na Wananchi katika kuadhimisha ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kimkoa yameadhimishwa katika Wilaya ya Kondoa.

Mhe. Senyamule amewashukuru na kuwapongeza viongozi na wakazi wa Wilaya ya Kondoa kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa kuupokea ugeni mzima wa mkoa wa Dodoma katika wilaya hiyo huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa chachu ya mafanikio kwa Wanawake hapa nchini na kuamini kwamba Wanawake wanaweza hata ukiangalia katika uteuzi wake wa viongozi ambapo wanawake wamepewa nafasi kwa kuamini usawa wa Kijinsia.

Hata hivyo, Mhe. Senyamule amewataka wanawake kujitokeza na kuzifanyia kazi fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na serikali ili kuweza kufikia malengo ya Usawa wa Kijinsia kwa maendeleo endelevu.

Ameongeza kwa kusema Jamii lazima izingatie haki za watoto wa kike na kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni ili aweze kufikia na kufaidi huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kupata elimu yenye kuwezesha kudai na kumlinda mtoto wa kike dhidi ya Ukatili wa Kijinsia.

Aidha Mkuu wa Mkoa aliwatunuku zawadi wanafunzi mbalimbali wa Wilaya zote za mkoa wa Dodoma waliofanya vizuri kwa kupata ufaulu wa daraja la kwanza  katika mitihani yao ya mwisho ya kidato cha nne mwaka 2022 ikiwa ni pamoja na kuzindua jukwaa la Wanawake na Samia Dodoma.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani imeadhimishwa duniani kote na katika Mkoa wa Dodoma maadhimisho yamefanyika katika Wilaya ya Kondoa ikipambwa na burudani mbalimbali na kwa mwaka huu yalibeba kaulimbiu isemayo “Ubunifu na Mabadiliko ya Technolojia, chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia.”

 

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya Katibu Muhtasi na Madereva Halmashauri ya Mji Kondoa February 24, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha nne Shule za Halmashauri ya Mji Kondoa January 29, 2023
  • Waliochaguliwa na shule walizopangiwa kidato cha kwanza 2023 Kondoa Mji December 14, 2022
  • Tangazo la kazi December 07, 2022
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mhe. Rais, Ditopile watoa milioni 15 kwa Wanawake wa Vikoba Kondoa

    March 13, 2023
  • "Shirikianeni watoro warudi shuleni"- Mkurugenzi Sweya

    March 09, 2023
  • RC Senyamule aongoza Wanawake wa Dodoma kuadhimisha siku yao Duniani

    March 08, 2023
  • Madaktari bingwa wawashauri wananchi kuchunguza afya mapema

    March 05, 2023
  • Tazama Vyote

Video

Fursa za uwekezaji Kondoa Mji
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa