• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wafanyabiashara wa nyama watakiwa kufuata taratibu

Tarehe iliyowekwa: September 8th, 2021

Wafanyabiashara ya nyama katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kufuata taratibu za uendeshaji wa biashara hiyo ili kuepuka kutoa faini ambayo itawaumiza katika biashara yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Paul Sweya wakati wa kikao kazi cha pamoja na wafanyabiashara hao kilichofanyika katika ukumbi wa kituo cha Uwekezaji Kondoa Mjini.

"Tunapofanya biashara tuzingatie masharti ya TMDA wakati mwingine inaumiza sana wanapokuja kufanya ukaguzi na mkabainika kuna makosa mnayo hali inayowapelekea kutoa faini kubwa wakati ni jambo dogo tu la kutimiza masharti sasa tukitoka hapa tukazingatie mapungufu na kuyafanyia kazi,"amesema Mkurugenzi Sweya

Aidha amewataka kufanya biashara na kuzingatia kuwa wao ni watoa huduma hivyo wasiwaumize wananchi katika bei wanazopanga na kuepuka upandishaji holela wa bei ya nyama.

"Sisi ni wamoja tuzingatie uzalendo na tutumie vikao kama hivi ili kujenga ushirikiano miongoni mwetu ili kuepuka kuonekana tofauti na kuwasihi kuwasikiliza na kuwaelewa maafisa kutoka bodi ya nyama ili kupata taratibu mbalimbali na kwenda kuzitekeleza," amesisitiza Mkurugenzi Sweya 

Kwa upande wake Dkt. Ocais Ngilisho kutoka Bodi ya Nyama aliwaeleza wafanyabiashara hao uwepo wa bodi ya nyama na sheria mbalimbali za nyama na umuhimu wake na kazi wanazofanya ikiwepo kutoa adhabu kwa wafanyabiashara wa nyama wanaokiuka sheria ya nyama.

"Sheria inakataza kuuza nyama bila kuwa na kibali kutoka bodi ya nyama na hii ni faida kwetu kwa kuwa unapotambulika inasaidia kuongeza masoko, kutambulika, kufuatiliwa na kuongeza kujiamini katika biashara zenu kwa wateja,"amesisitiza Dkt. Ngilisho

Hata hivyo aliwashauri wafanyabiashara hao ambao hawana vibali kukata vibali na ambao vibali vimeisha kuhuisha vibali vyao na kuwashauri kuunda umoja wao ili kiweza kupata fursa mbalimbali zinazopatikana katika bodi ya nyama ambapo inakuwa vigumu kuzitoa kwa mtu mmoja mmoja.

Akifunga kikao kazi hicho Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji Kondoa Monica Kimario amewataka wafanyabiashara hao kwenda kubadilika kwa kujenga mabucha ya kisasa ili kuendana na ukuaji wa mji na kuwa waaminifu katika nyama wanazouza kwa kuhakikisha zimekaguliwa na wataalam wa mifugo.

Kwa upande wao wafanyabiashara hao wameishukuru Halmashauri kwa kuandaa kikao kazi hicho na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi waliyoelekezwa na kuomba kupata vikao hivyo vya uelewa mara kwa mara kwani lengo lao ni kihakikisha wanalipa kodi za serikali ili kufanya biashara yao kwa kujiamini.

Kikao kazi kati ya wafanyabiashara wa nyama kimefanyika kwa lengo la kukumbusha taratibu mbalimbali za biashara ya nyama ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na wataalam wa Idara ya Mifugo na Uvuvi na kuhudhuriwa na wataalam kutoka Bodi ya Nyama Dodoma.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa