• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wasiowapeleka watoto shule, wanaotembea na wanafunzi waonywa

Tarehe iliyowekwa: November 16th, 2023

Wasiowapeleka watoto shule na wanaotembea na wanafunzi katika Wilaya ya Kondoa wametakiwa kuacha tabia hiyo haraka kwani kwa kufanya hivyo wanaongeza idadi ya utoro mashuleni na kuwanyima haki ya elimu watoto na kuua ndoto zao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi katika kata za Serya na Kingale baada ya diwani wa kata ya kuwasilisha changamoto ya watu wazima kutoka kimapenzi na wanafunzi hivi karibuni.

“Mnaowanyemelea watoto wetu mjiandae tutakwenda kuongea na wanafunzi watutajie wanaotoka nao mtu ukitajwa sheria lazima ichukue mkondo wake na tutakupeleka moja kwa moja mahakamani na hatutakuwa na mswalie mtume katika jambo hilo kwanini msiwafuate watu wazima wenzenu,”amesema Dkt. Mkanachi

Aidha amesema wazazi pia wasiowapeleka watoto shuleni kwa mwaka wa masomo unaotarajia kuanza Januari 2024 wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kulipa faini na kuwaagiza watendaji kusimamia jambo hilo ili kila mtoto aliyemaliza darasa la saba anakwenda kidato cha kwanza na anamaliza hadi kidato cha nne.

“Pia wazazi wote wenye watoto mlime na mzalishe chakula cha kutosha na mpeleke chakula shuleni ili watoto wapate chakula shuleni na waweze kusoma kwa utulivu na kuondoa utoro kwa wanafunzi na nawaomba viongozi wa dini mtusaidie katika hili la kumaliza utoro kwa wanafunzi shuleni,”amesisitiza Dkt. Mkanachi

Aidha amewaagiza maafisa ugani wote kuhakikisha wanafanya mikutano na wakulima ili kuwapa utalaam wa namna ya kulima kisasa ili waweze kuzalisha kwa wingi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawapatia mbegu na mbolea za ruzuku kwa wakati na kuwahakikishia wananchi kuwa hawatapata tabu tena ya mbolea na mbegu za ruzuku kwani vitafika kwa wakati.

“Lakini pia kwa wakulima nyie nawaomba mhakikishe mnaomba mbolea ya ruzuku kwenye mfumo ambao ndio utaratibu wa sasa muufuate mapema utaratibu huo ili taratibu zingine zifuate ikiwemo kuagiza mbolea na mbegu kutoka kwa wakala mkuu aliyepo mkoani Dodoma,”amesema Dkt. Mkanachi

Wakitoa changamoto zao katika mikutano hiyo Mhe. Kulwa Pazi Diwani kata ya Serya na Mhe. Abushehe Mbuva Diwani kata ya Kingale wamesema kata zao zina changamoto kubwa katika  sekta ya maji na umeme pamoja na kazi kubwa iliyofanywa na serikali katika kuwapatia huduma hizo katika baadhi ya mitaa.

Aidha wamemashukuru Rais Dkt. Samia Suhulu Hassan kwa kuwaletea miradi mingi kwa kipindi kifupi ikiwemo barabara, madarasa, nyumba za walimu, zahanati na vituo vya afya, visima vya maji ambavyo vinangojea kupata fedha kwa ajili ya usambazaji katika maeneo ya watu.

Ziara ya Mkuu wa Wilaya imefanyika katika kata ya Kingale na Serya kwa kuongea katika mikutano ya wananchi ambapo waliwasilisha kero mbalimbali na aliongozana na wataalam kutoka Halmashauri ya Mji na taasisi za kiserikali ikiwa ni muendelezo wa kusikiliza kero za wananchi katika kata zote 29 za Wilaya ya Kondoa ambapo hadi sasa ameshasikiliza na kuzitatua kero za wananchi wa kata 19.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Wasira aelezea faida za Muungano kwa wananchi wa Kondoa

    April 26, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa