• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Baraza la Madiwani Kondoa Mji 2016-2020 lajivunia kuongeza mapato

Tarehe iliyowekwa: June 10th, 2020

Hatimaye Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kondoa limekamilisha rasmi kikao cha kawaida cha robo ya nne baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano tangu lilipoingia madarakani mwezi Oktoba 2015 na kufanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka  shilingi milioni 400 kwa mwaka 2016/2017 hadi kufikia shilingi bilioni 1.6 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la zaidi ya  asilimia 135.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa katika kikao  cha  kawaida cha kuvunja Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Kuongezeka kwa mapato kumetokana na usimamizi mzuri wa Waheshimiwa Madiwani katika matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato wa Serikali za Mitaa unaotumia mashine za kukusanyia mapato “POS”,alisema Mkurugenzi Dakawa.

Aidha  katika upande wa rasilimali fedha Mkurugenzi amesema kuwa Halmashauri imeendelea kufanya vizuri katika usimamizi wa matumizi ya fedha na ufungaji wa hesabu kulikopelekea kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo  kutokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

“ Uongozi ni dhamana na kipimo cha utumishi ni jinsi ambavyo tunaweza kusimamia utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo, hivyo nawaomba watumishi wote kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana katika kusimamia maendeleo na kuibua vyanzo vipya vya mapato,pia ninaawashukuru sana Waheshimiwa Madiwani kwa utendaji kazi wenu mzuri toka mwanzo hadi mwisho mmefanya  kazi kubwa ya kuleta maendelao  kwa Halmashauri yetu kwa uzalendo na uvumilivu,” alisisitiza Mkurugenzi  Dakawa.

Akielezea mikakati iliyowekwa na Halmashauri katika ukusanyaji wa mapato alisema kuwa Halmashauri imewekeza katika miradi mkakati itakayotumika kama vyanzo vya mapato kama vile ujenzi wa stendi ya mabasi na Malori Bicha, ujenzi wa machinjio Bicha pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Aidha Mwenyekiti waHalmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Hamza Mafita alimshukuru  Mkuu wa Wilaya Mhe. Sezaria Makota, Mkurugenzi, Waheshimiwa Madiwani, Viongozi wa Chama pamoja na wakuu wa Idara kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati wote wa uongozi wake.

“Tuliamua fedha za TARURA zijenge barabara mjini  kwa kiwango cha lami kila mwaka angalau kilomita moja na nusu, pia tumeomba tuongezewe  mifereji na taa za  Barabarani.Hali kadhalika tumejitahidi kupunguza kero ya maji kwa wananchi kwa kuleta mashine mbili ambazo zitasaidia upatikanaji wa maji kwa wingi  kikubwa zaidi najivunia Uongozi wangu hatujawahi kupata hati chafu  hii yote inamaanisha tumesimama imara.

Baraza la Waheshmiwa Madiwani Halmashauri ya Kondoa mji limehairishwa rasmi  ambapo mgeni rasmi katika  baraza hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe Sezaria Makota  na kuhudhuriwa na  Waheshimwa madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Wakuu wa Idara na vitengo pamoja na wananchi.  

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa