• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Bilioni 2.3 zang'arisha sekta ya afya Kondoa Mji

Tarehe iliyowekwa: November 1st, 2023

Zaidi ya shilingi bilioni 2,365,005895 zimeletwa na Serikali ya awamu ya sita katika Halmashauri ya Mji Kondoa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ikiwemo ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa vifaa tiba.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Paul Mamba Sweya wakati wa mkutano na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutangaza mafanikio ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mikoa na halmashauri iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

“Kwa kuona umuhimu wa uwepo wa vituo vya afya Serikali ya awamu ya sita imeleta shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Serya baada ya kusikia kilio cha wakazi wa kata hiyo ambapo mwaka 2021 mzazi mmoja alifariki na mtoto wake wakati akijifungua kutokana na kujaa maji kwa Mto Bubu unaounganisha kata hiyo na Kondoa Mjini ilipo hospitali kubwa,”amesema Mkurugenzi Sweya.

Ameongeza kuwa Serikali pia imeleta shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kolo na imeongeza idadi ya vituo vya afya kutoka kituo kimoja hadi kuwa na vituo vya afya 3 ambavyo vimesaidia kupunguza msongamano katika Hospitali ya Mji.

“Pia Serikali imeleta zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika mitaa sita na kupelekea kuongezeka kwa zahanati kutoka 4 hadi kufikia zahanati 10 ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo ambapo wananchi walikuwa wakisafiri zaidi ya kilomita 10 kutafuta huduma za afya,”amesisitiza Mkurugenzi Sweya

Ameendelea kueleza kuwa serikali kwa kuona Hospitali ya Mji ni chakavu wameleta shilingi milioni kwa ajili ya ukaratabati wa majengo ya hospitali hiyo ambapo majengo mapya ya kisasa matatu yamejengwa ambayo ni jengo la upasuaji, mama na mtoto na jengo la mochwari

“Pia kwa upande wa vifaa tiba imeleta shilingi milioni 1,265,468,504.2 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali ya Mji na vituo vya kutolea huduma za afya ambapo kwasasa vipimo vingi vinafanyika katika maeneo hayo na watumishi wanapata ujuzi zaidi kutokana na kutumia vifaa hivyo vya kisasa,”amesema Mkurugenzi Sweya

Akitaja manufaa ya miradi hiyo amesema kuwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za barabarani na magonjwa ya dharura, kupunguza vifo   vya  mama na mtoto vitokanavyo na uzazi, kuongeza morali ya kazi kwa watumishi   kufuatia uwepo wa nyumba za watumishi na  uwepo wa vifaa tiba vya kisasa, kusogeza huduma za afya karibu na wananchi   ambapo awali  walilazimika kusafiri  umbali mrefu  kupata huduma za Afya. 

Kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya kauli mbiu “Tumekusikia Tumekufikia” imezinduliwa katika mkoa wa Dodoma ambapo imefunguliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kufungwa na Naibu Waziri wa OR TAMISEMI Mhe. Festo Ndugange na imehudhuriwa pia Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Mobhare Matinyi, Mhe. Rosemary Senyamule Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Dodoma.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa