• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kamati ya Fedha wapongeza mapato ya ndani kutekeleza miradi ya maendeleo

Tarehe iliyowekwa: April 18th, 2025

Kamati ya Fedha na Utawala Halmashauri ya Mji Kondoa imempongeza Mkurugenzi kwa kupelekeka fedha kiasi cha shilingi milioni 198 zitokanazo na mapato ya ndani kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo itawasaidia wananchi kupata huduma muhimu kwa ukaribu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji KondoaM he. Mohamed Kiberenge wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi robo ya tatu ambapo kamati hiyo ilitembelea miradi mbalimbali ili kuona utekelezaji wake ambapo pia waliongozana na Wakuu wa Idara.

“Mapato yetu ni kidogo lakini mmepambana kuhakikisha fedha zinapelekwa kwenye miradi tunawapongeza sana lakini pia tunashauri muongeze usimamizi kuhakikisha fedha zote zilizotolewa zinatekeleza kazi iliyokusudiwa na miradi inakamilika kwa wakati uliopangwa,”amesema Mhe. Kiberenge

Aidha ameshauri kuendelea kupeleka fedha kwenye miradi viporo ili ikamilike badala ya kuanza utekelezaji wa miradi mipya na kuwashukuru watumishi kwa ushirikiano wao wakati wa utekelezaji wa miradi ambayo mingi imekamilika na ipo katika viwango vizuri na ana Imani iradi hiyo itakamilika kwa wakati.

Wakiongea kwa katika miradi ya Suruke na Amali Kingale wajumbe wa kamati ya fedha wamepongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo na hatua iliyofikiwa na kushauri wasimamizi kufuata taratibu zote za manunuzi wakati wa utekelezaji wa mradi na kuepuka kuzalisha madeni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa ameishukuru kamati kwa ushauri wao na kuwahakikishia kuwa miradi yote itakamilika kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha kukamilika na kuendelea kupeleka fedha kwenye miradi iliyosalia kama ilivyopangwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.

“Mhe. Mwenyekiti wa wajumbe wote niwahakikishie kuwa miradi hii itakamilika kwa wakati na hakuna mradi ambao utavuka na fedha ukiacha miradi michache ambayo kuna marekebisho ya vifungu na tumeambiwa itawekwa kwenye bajeti ijayo lakini mingine yote itakamilika kwa wakati,”amesisitiza Mkurugenzi Majaliwa

Kamati ya Fedha na Utawala imefanya ukaguzi wa miradi kwa robo ya pili ambapo imekagua miradi ya ujenzi wa Sekondari Suruke, Shule ya Amali Kingale, nyumba ya  mganga Zahanati ya Kichangani, Ofisi ya Mtaa wa Tumbelo, Zahanati ya Mulu na umaliziaji wa Ofisi ya Mtaa Wis kwa Ntisi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa