• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kamati ya siasa mkoa yaridhishwa na ujenzi Bolisa Sekondari

Tarehe iliyowekwa: November 13th, 2023

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi na Mjumbe wa kamati ya siasa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma Ndg. Samweli Malecela amesema kamati ya siasa mkoa imeridhishwa na ujenzi wa Shule ya Sekondari Bolisa na  amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Mji Kondoa kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanywa na kamati ya siasa mkoa wa Dodoma ikiwa imeongozana na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kondoa na wakuu wa divisheni na vitengo wa Halmashauri ya Mji Kondoa.

Aidha amesema awali majengo mazuri kama ya Sekondari yalikuwa yanaombewa kuwa chuo kwa watu kudhani wanafunzi wa vidato vya chini hawastahili kuwa na majengo mazuri lakini serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi na sasa shule zote zinamuonekano mzuri na wameweka nia ya kuhakikisha kila mtoto anasoma mazingira mazuri kama ya shule ya Sekondari Bolisa.

Aidha ameutaka uongozi wa Halmashauri kuhakikisha fundi nayejenga maabara anasimamiwa na anamaliza mapema maeneo yaliyobakia ili wakati ukifika shule hiyo ianze kuchukua wanafunzi kama ilivyopangwa.

Aidha ameongeza kuwa amelichukua ombi la Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kondoa Mhe. Hija Sulu la kuomba kujengewa shule ya sekondari katika kata ya Suruke ikiwa ndio kata pekee iliyobakia kuwa na sekondari na kuwataka kuendelea kuwaza kujenga shule ya kidato cha tano na sita.

Akiongea katika eneo la mradi diwani wa kata ya Bolisa Mhe. Ramla Abeid ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwaletea mradi huo ambao ulikuwa hitaji kubwa la wananchi  wa kata hiyo kwa kuwa watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu hadi Gubali Sekondari kufuata elimu ya Sekondari.

“Pia namshukuru sana Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipa miradi kata ya Bolisa ambapo pia nimeambiwa ameleta shilingi milioni 69 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu ambao haujaanza  katika Shule ya Sekondari Gubali ambayo inalelewa na kata hii ya Bolisa hatuna cha zaidi cha kumpa zaidi ya shukrani,”amesema Mhe. Ramla

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Paul Sweya amewashukuru viongozi wa chama ngazi ya mkoa na wilaya kwa kufanya ziara katika mradi huo kwani kwa kufanya hivyo kunawasaidia kuona makosa ambayo wenyewe hawawezi kuyaona na kuahidi kuufanyia kazi ushauri walioutoa na kukamilisha ujenzi kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Shule ya Sekondari Bolisa ilianza ujenzi mwezi Agosti baada ya kupokea fedha kutoka Serikali kuu zaidi ya shilingi milioni 540 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa7, maabara 3, jengo la ICT, maktaba, jengo la utawala, matundu 10 ya vyoo na hadi sasa zaidi ya shilingi milioni 530 na kukamilika kwake kutawapunguzia umbali wanafunzi kutembea zaidi ya kilomita 8 kufuata elimu ya Sekondari.














Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa