• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kamati ya Ushauri ya Wilaya yakutana kujadili mpango na bajeti ya mwaka 2025/2026

Tarehe iliyowekwa: January 25th, 2025

Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Kondoa imekutana na kujadili mpango na bajeti ya Halmashauri ya Mji Kondoa kwa mwaka wa fedha 2025/2025.

Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Nyangasa kimefanyika katika ukumbinwa mikutano wa Halmashauri ya Mji Kondoa.

Akiongea katika kikao hicho Mhe. Fatma amewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Mji Kondoa wakiongozwa na Mkurugenzi kwa usimamizi mzuri wa fedha zinazoletwa na Serikali na kuwataka kuendelea kusimamia ili zitimize malengo ya Serikali.

Aidha amewataka kuhakikisha kuwa wanaendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato ikiwa ni pamoja na kuangalia vyanzo ambavyo vipo nyuma ili kuina namna ya kuweka njia sahihi ya kukwamua changamoto za kutofikia malengo ya ukusanyaji.

"Bajeti ni nzuri hivyo tukafanye kazi ili dira yetu ya Halmashauri inavyosema na tukue kimapato na kuimarisha uchumi wa wananchi" amesisitiza Mhe.Fatma

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg.Said Majaliwa amewashukuru wajumbe kwa michango yao na kuahidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa kwa maendeleo ya wanakondoa.

"Ushauri wenu tumeuchukua tutaona namna ya kuufanyia kazi na wataalam na ndio maana ya kukaa nanyi wajumbe wa kikao hiki ili kushauri sehemu ambayo sisi hatukuona,"amesisitiza Mkurugenzi Majaliwa

Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Damas Masanja amesema kwa kipindi cha mwaka 2025/2026 Halmashauri imepanga kukusanya shilingi bilioni 22,268,656,964.31 kutoka vyanzo vya ndani, ruzuku kutoka Serikali kuu na wahisani.

Kikao cha Ushauri Wilaya kimeketi kwa ajili ya kujadili mpango na bajeti 2025/26 ikiwa ni kwa mujibu wa Sheria ili kupata maoni ya wadau mbalimbali na kimehudhuriwa na Kamati ya Usalama, Mwenyekiti wa Halmashauri, mbunge wa Kondoa Mji Mhe. Ally Makoa, Wakuu wa Idara na Vitengo, viongozi wa dini, Wakuu wa Taasisi, Wawakilishi wa Vyama vya Siasa, Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata.



Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa