• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Kingale Shirikianeni"- Dkt. Binilith

Tarehe iliyowekwa: September 3rd, 2018

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amewataka wananchi wa Kata ya Kingale kushirikiana pamoja katika ujenzi wa Kituo cha Afya Kingale kwani huduma itakayotolewa itawanufaisha wote.

Aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika kata ya Kingale eneo linalojengwa kituo cha Afya na kufanya mkutano wa hadhara hivi karibuni.

"Fedha zinetolewa Na Rais Dkt John Magufuli kwa ajili ya kuboresha huduma za afya jambo ambalo litawapunguzia umbali wa kufuata huduma mjini kwa kumuunga mkono Rais shirikianeni kukamilisha kituo hiki."Alisema Dkt. Mahenge

Aliongeza kwa kuwataka viongozi wa mitaa ambayo haijachangia kwenda kuitisha mikutano Na kuwahamasisha wananchi kuchangia ujenzi kama mitaa mingine kwani ugonjwa ukija hauangalii chama, urefu wala kabila la mtu.

Awali akiongea katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Sezaria Makota alisema kuwa wananchi wa Kingale ni wapenda maendeleo Na ni moja ya kata zinazoongoza katika elimu na uchangiaji wa CHF na juhudi zao zimeonekana katika ujenzi wa kituo cha afya ambapo wameshachangia tofali, mchanga na mawe ambavyo vipo eneo la ujenzi tayari.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Issa Ramadhan alisema kuwa mradi huo uliibuliwa na na wananchi na jumla ya majengo matano yatajengwa ikiwemo nyumba ya mganga ambapo serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 400 na wananchi wanatarajia kukusanya jumla ya shilingi milioni 15 na hadi sasa wamechangia shilingi milioni 11.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma amefanya ziara katika wilaya ya Kondoa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea wilaya za mkoa wa Dodoma ambapo Kondoa alikagua miradi ya maendeleo na kuahidi kutoa shilingi milioni moja na nusu na kuchangisha shilingi milioni moja na laki nne kutoka kwa viongozi wa serikali alioongozana nao kwenye ziara yake kuunga mkono nguvu za wananchi wa Kingale.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa