• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Mji wapongezwa kulipa deni la Madiwani

Tarehe iliyowekwa: June 3rd, 2020

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Kessy Maduka ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mji Kondoa kwa kulipa deni la Waheshimiwa madiwani na kupelekea Halmashauri hiyo kubakia na deni la miezi miwili.

Pongezi hizo alizitoa wakati wa baraza maalum la kupitia na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mitaa katika ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Mkuu wa Mkoa anaiunga mkono Halmashauri ya Mji Kondoa na ameniagiza niseme kuwa ni moja ya Halmashauri ambazo hana shida nazo maana mmeshaweza kujiongoza wenyewe na kulipa deni la waheshimiwa madiwani kwa wakati ambapo katika mkoa ni halmashauri tatu tu zilizofikia hatua hiyo,”alisema Kessy

Aidha aliongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na mshikamano katika ukusanyaji mapato na kupelekea kuthubutu kupandisha mapato mara dufu ambapo ni halmashauri chache sana zenye kufanya uthubutu huo.

Hata hivyo alitilia mkazo mambo mbalimbali ili kuboresha zaidi utendaji kazi kwa kuimarisha masuala ya mapato ya ndani na vyanzo vyake, kulipa madeni ya watumishi, kusimamia kesi za halmashauri kwa ukaribu ili kulinda mali za serikali zisipotee na kuyaandikia taarifa magari chakavu ili TEMESA wayakague na kuuzwa ili kununua magari mengine.

Akiongea  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Hamza Mafita alimshukuru Katibu Tawala kwa pongezi alizozitoa na kumuahidi kuendelea kufanyakazi kwa umoja na mshikamano ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma na kwa wakati.

“Tutamaliza deni letu kwa wakati tumebakisha miezi miwili fedha inayolipwa ndani ya wiki hii na mafanikio hayo yametokana na mshikamano uliopo kati ya Wakuu wa Idara, Mkurugenzi. Waheshimiwa madiwani na Mkuu wa Wilaya na panapotokea tofauti tunakaa chini na kuzimaliza kwa hoja,”alisisitiza Mhe. Mafita

Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa Mkoa wa Dodoma Sesemka Chambi aliipongeza Halmashauri kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo na kuwashauri kutobweteka ila kuendelea kuzitetea kwa kuhakikisha wanafuata sheria, taratibu na kanuni za fedha ili kuepukana na kupata hati chafu hapo baadae.

Baraza maalum la Waheshimiwa Madiwani liliketi kwa ajili ya kujadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mitaa katika ukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2018/2019 na kupelekea Halmashauri kupata hati safi kwa mwaka wa tatu mfululizo na lilihudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa, Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za mitaa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, viongozi kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Dodoma na Wakuu wa Idara.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa