• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kondoa Washukuru Mradi wa SAUTI

Tarehe iliyowekwa: October 17th, 2018

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Kaunga Amani amewashukuru viongozi wa mradi wa SAUTI  kwa kutambulisha mradi huo katika mji wa Kondoa kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa mji huo.

Pongezi hizo alizitoa wakati wa kikao cha kutambulisha mradi huo kwa watumishi wa idara ya afya wa halmashauri ya Mji wa Kondoa na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa katika ukumbi wa jengo la biashara Kondoa Mjini.

Alisema kuwa Mji wa Kondoa unakua kwa kasi kubwa hivyo kuleta mradi huo wa kuwafikia watu walio kwenye hatari ya kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi  na kuwafanya wakatambua hali zao ni jambo jema sana kwani itasaidia sana katika kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi katika mji mdogo wenye mwingiliano mkubwa wa watu.

“Nashauri msiishie katika kuyafikia makundi hayo tu bali kwa pamoja tutengeneze mazingira ya kuhakikisha wanaogundulika na maambukizi hawasambazi maambukizi mapya kwa watu wengine ili kuunga mkono jitihada za serikali za kufikia tisini tatu katika kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi”. Alisema Kaunga

Aidha aliwataka waganga wakuu wa halmashauri zote za Kondoa kuonyesha ushirikano kwa wadau hao wa afya ili kuhakikisha lengo la mradi linafikiwa na kuwasihi timu ya mradi kufika ofisi ya mkurugenzi wanapokumbana na changamoto katika kazi zao ili waweze kutatua kwa pamoja.

Akiongea Meneja wa Mradi wa SAUTI Dr. Raymond Bandio amesema mradi huo umeletwa Kondoa ili kuyafikia makundi yaliyo katika hatari ya kuambukizwa  Virusi Vya Ukimwi  kwa kutoa ushauri nasaha na kupima Virusi vya Ukimwi ikiwa ni pamoja na kugawa kondomu ili kupunguza kasi ya maambukizi mapya.

“Tumelenga kuzifikia 90 mbili kati ya tatu za mkakati wa serikali wa kuzifikia 90 tatu katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi ambapo  tutahakikisha watu  wanatambua hali zao kiafya na wataokutwa na maambukizi tutahakikisha wanaanza kutumia dawa za kufubaza Virusi Vya Ukimwi  na hatuchagui maeneo ya kazi tutafika majumbani, nyumba za starehe na sehemu za maofisini ili kutoa huduma.” Alisisitiza Dr. Raymond

Aliongeza kwa kuzitaja kata ambazo zitapata huduma hiyo katika halmashauri ya Mji Kondoa kuwa ni Chemchem, Kingale na Kondoa Mjini ambapo katika halmashauri ya wilaya ya Kondoa huduma hii itatolewa katika kata za Pahi, Bumbuta, Busi, Changaa, Haubi, Itaswi, Kalamba, Kikore, Kisese,Kwadelo na Mnenia.

Mradi wa SAUTI umeanza kazi ya kuyafikia makundi maalum yaliyo katika hatari ya kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi  katika Wilaya ya Kondoa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu hadi Septemba mwakani ambapo wamejiwekea malengo ya kuwafikia watu 10,863 ikiwemo 7,010 watu wazima, 3853 watoto aidha imejipanga kuwafikia WAVIU 1998 na 90 watoto wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kuhakikisha wagonjwa 1898 wanaunganishwa na huduma za CTC.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa