• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kotumo watakiwa kutokatishwa tamaa ujenzi wa Zahanati

Tarehe iliyowekwa: May 4th, 2021

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Dakawa amewataka wananchi wa Kotumo katika Mtaa wa Hachwi kutokatishwa tamaa na mtu yoyote asiyependa maendeleo katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Zahanati unaoendelea katika eneo lao. 

Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa wananchi wa kata uliofanyika katika eneo la Kotumo na kuhudhuriwa pia na Mheshimiwa diwani wa kata ya Kolo.

"Kondoa ni wilaya ya zamani sana imeanza pamoja na Nairobi lakini ukifananisha ni vitu tofauti utaona sisi tumechelewa sana na hii inawezekana kabisa kuna watu walisababisha turudi nyuma sasa watu hao tuwakatae kabisa wale wanaotaka kutuletea maendeleo tuambatane nao kwasababu tunataka maendeleo,"amesema Mkurugenzi Dakawa.

Aidha ameongeza kuwa si jambo jema kuona mama mjamzito au mzee atoke katika milima yote hii aende akatibiwe Bolisa au Kolo na wao wakashindwa kujenga Zahanati jambo ambalo si jema na kuwapongeza wananchi hao kwa kuanza kujenga Zahanati ikiwa wananchi wengine wakijitoa kujenga.

"Nimeambiwa kuwa hapa kuna mgogoro mkubwa kuwa kuna Warangi na Wasi na mmesahau kuwa sisi wote ni watanzania na Hayati Mwalimu Nyerere aliweza kutuunganisha makabila yote tukawa kitu kimoja bila hivyo tusingeweza kuja kufanyakazi Kondoa kwa kuwa si wenyeji wa Kondoa lakini tumekuja kwa kuwa wote ni pamoja," amesisitiza Mkurugenzi Dakawa

Hata hivyo amewasihi wananchi hao kushirikiana kwa pamoja katika kukamilisha Zahanati hiyo na kutokubaliana na mtu yoyote atakayetaka kuwarudisha nyuma na kuwataka kutokata tamaa ndio maana amefika kuwatia moyo katika jambo lao la maendeleo na kuacha wasiopenda maendeleo wapige kelele na wao wawajibu kwa vitendo kwa kufanya kazi.

"Nakuagiza Mtendaji wa kata kuwafikisha katika baraza la kata wananchi wote ambao hawatatoa mchango na watozwe faini ambazo pia ziletwe kuchangia katika mradi huu na tunafanya hivi kwa kuwa jambo hilo lipo kisheria,"amemaliza Mkurugenzi Dakawa

Akiongea Mheshimiwa Diwani wa kata ya Kolo Mhe. Idd Ng'ungu ameishukuru serikali kwa kuwaletea fedha za ujenzi wa Zahanati pamoja na ujio wa Mkurugenzi na wataalam wake ambapo pia amewataka wananchi kutokata tamaa kwa kuwa wapo pamoja katika ujenzi huo hadi utakapokamilika.

Naye mwakilishi wa wananchi Salimu Bura ameahidi kuwa mradi utakamilika kwa wakati kwa kuwa wananchi wote wa Kotumu ujenzi huo kwao ni kama mboni ya jicho kutokana na shida wanazopata kufuata huduma za afya.

Ziara ya kuhamasisha utekelezaji wa maendeleo imeanza leo ambapo Mkurugenzi na wataalam mbalimbali wanafanya mikutano ya mitaa mbalimbali kuwahamasisha wananchi kujitoa katika utekelezaji wa miradi ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya afya na elimu katika kata zote nane za Halmashauri ya Mji Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa