• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Ustawi wa Jamii
    • Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Madaktari bingwa wawashauri wananchi kuchunguza afya mapema

Tarehe iliyowekwa: March 5th, 2023

Wananchi wa Halmashauri ya Mji Kondoa na maeneo ya jirani wameshauriwa kuwa na mwamko wa kufanya uchunguzi wa afya zao mapema ili wanapogundulika na tatizo waweze kuanza tiba mapema.

Ushauri huo umetolewa na Dkt. Peleus Kato kwa niaba ya madaktari bingwa waliofika katika Hospitali ya Mji Kondoa kutoa huduma za matibabu kwa muda wa wiki moja hivi karibuni.

“Wananchi wengi wanagundua ugonjwa wakati umefika mbali sana hali inayopelekea kuwa vigumu kupata matibabu na hii inachangiwa na kuwa wengi wetu hatuna utamaduni wa kupima afya zetu mapema tunakuja kushtuka hatua ambayo usumbufu wa ugonjwa umeanza.”Amesema Dkt. Kato

Aidha amesema katika kipindi chote walichokuwa wakitoa huduma mwitikio wa wananchi umekuwa ni mzuri na wamefanikiwa kutoa huduma zote muhimu ikiwemo ushauri, matibabu na kufanya upasuaji kwa waliokidhi vigezo na ambao wamegundulika na matatizo zaidi kulingana na mazingira wamepewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu zaidi.

“Tutawasiliana na uongozi wa Hospitali tumeona matatizo kwa akinamama ambako foleni ni kubwa hivyo tutaona jinsi gani ya kufanya ili angalau kliniki kama hizi zisiwe zinakaa kipindi kirefu bila kufanyika  zinaweza kupangiwa wataalam wachache wakawa wanakuja ili kuwasaidia wananchi,”amesisitiz Dkt. Kato

Kwa upande wake Ndg. Salehe Kadete Kaimu Mganga Mkuu amewashukuru madaktari hao kwa ujio wao kwani wamesaidia kwa kiasi kikubwa kwani wananchi wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za kufika Dodoma kwa ujio wao wamewasogezea huduma hivyo wamewapunguzia gharama kwa kiasi kikubwa.

“Hata hivyo pamoja na kusogeza huduma lakini pia mmewajengea uwezo watumishi wetu naamini kuna vitu vipya vingi wamejifunza wao wanafanya kazi hapa kila siku hivyo wakati mwingine wanafanya kwa mazoea na kwasasa mambo yanabadilika kila siku hivyo wataongeza utaalam na tutarajie kuona ufanisi ukiongezeka,”amesisitiza Kadete

Akiongea awali Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dkt. Frolence Hilary amesema Hospitali ipo katika hali ya maboresho ambapo serikali ilitoa shilingi milioni 900 kwa ajii ya ukarabati wa Hospitali ambapo ujenzi unaendelea hivyo wakifika kwa wakati mwingine watakuta miundombinu imeboreshwa kwa kiasi kukubwa na wataweza kutoa huduma katika mazingira rafiki zaidi.

Huduma ya matibabu kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Rufaa Dodoma na Benjamini Mkapa imefanyika kwa kipindi cha wiki moja ikiwa ni sehemu ya mpango wa Hospitali kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi na jumla ya wagonjwa 114walifanyiwa upasuaji mkubwa na mdogo.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya Katibu Muhtasi na Madereva Halmashauri ya Mji Kondoa February 24, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha nne Shule za Halmashauri ya Mji Kondoa January 29, 2023
  • Waliochaguliwa na shule walizopangiwa kidato cha kwanza 2023 Kondoa Mji December 14, 2022
  • Tangazo la kazi December 07, 2022
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mhe. Rais, Ditopile watoa milioni 15 kwa Wanawake wa Vikoba Kondoa

    March 13, 2023
  • "Shirikianeni watoro warudi shuleni"- Mkurugenzi Sweya

    March 09, 2023
  • RC Senyamule aongoza Wanawake wa Dodoma kuadhimisha siku yao Duniani

    March 08, 2023
  • Madaktari bingwa wawashauri wananchi kuchunguza afya mapema

    March 05, 2023
  • Tazama Vyote

Video

Fursa za uwekezaji Kondoa Mji
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa