• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Mkiamua hisabati si ngumu"- DC Mkanachi

Tarehe iliyowekwa: September 27th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amewataka walimu wa somo la hisabati shule za msingi Kondoa kuamua kufundisha kwa dhati na kwa kujitoa zaidi kwa kuwa somo hilo siyo gumu kama wanavyodhani.

Ameyasema hayo wakati akiongea na walimu wa somo la hisabati wanaopatiwa mafunzo ya uboreshaji ufundishaji wa somo hilo yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kondoa Irangi ambayo yanafadhiliwa na programu ya Shule Bora.

"Niwaambieni jambo ambalo wengi mnalikosa walimu wengi hamna muda na wanafunzi, sina shida na nyie kufanya mambo yenu binafsi ila shida yangu ni commitment yenu kwa wanafunzi siioni,"amesema Dkt. Mkanachi

Amesema walimu wengi wapo shuleni kuhakikisha wanafundisha tu kwa mujibu wa ratiba kwa kuwa inamtaka afundishe lakini si kwa ajili ya wanafunzi kuelewa jambo ambalo linafanya watoto wasielewe somo hilo.

"Sasa naomba walimu wenzangu mkitaka kweli watoto wafaulu mnaweza na inawezekana kama mwalimu ukitaka utafanya kila mbinu kuhakikisha mwanafunzi anafaulu lakini walimu wasasa wengi hamjiongezi na hamjali mwanafunzi afaulu au asifaulu,"amesisitiza Dkt. Mkanachi

Ameongeza kuwa walimu wasasa wengi hawajitumi hata wanapokuwa darasani anapojua mwanafunzi huyu atafeli hajali jambo siyo ualimu ukilinganisha na walimu wengi wa zamani.

"Kuwashirikisha wanafunzi itatusaidia kuleta matokeo  mahusiano mazuri na wanafunzi na kuwajua kwa uwezo wao na majina yao ili wenye uwezo mdogo ujue utawasaidia kwa namna gani, lakini mwalimu wa leo ukimwambia akutajie majina hata robo tatu ya darasa hawezi atamjua monita tu wengine hawezi,"amesema Dkt. Mkanachi

Amewaambia walimu hao kuwa ili wafaulishe na kufanya vizuri lazima waamue wenyewe kwanza kwa kuwa hata wakifundishwa kwa semina za namna na mbinu zote msipoamua matokeo yatabakia vilevile na hawa wawezeshaji watabakia kuwa mashahidi tu kuwa walishawafundisha.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Kondoa Ndg. Christina Kalekezi amewatia moyo walimu kuwa wanaweza na wao ndio walimu wa msingi hivyo wakifanya vizuri katika hesabu msingi huo wataenda nao hadi sekondari lakini wakifanya vibaya itakuwa ni ngumu kwa Sekondari.

Akishukuru wa niaba ya walimu wenzie Mwalimu amesema wanashukuru kwa mafunzo hayo na watakwenda kuyafanyia kazi yote waliyofundishwa na matokeo yataonyesha mabadiliko.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo yanayofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi kwa kuwashirikisha walimu 50 wa somo la hisabati kutoka shule za msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ili kuinua ufaulu wa somo hilo.



Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Wasira aelezea faida za Muungano kwa wananchi wa Kondoa

    April 26, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa