• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Timizeni wajibu mdai haki"- Mkurugenzi Sweya

Tarehe iliyowekwa: June 21st, 2023

Watendaji wa kata na mitaa katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kutimiza wajibu wao kama watumishi wa serikali ndipo wadai haki kwani bila kufanya hivyo hawaitendei haki Serikali inayowalipa mishahara kwa kila mwezi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Paul Sweya wakati wa kikao kazi cha pamoja kati yake na Watendaji wa kata na mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji hivi karibuni.

“Asiwepo mtumishi anayesema hafanyi kazi bila kupewa motisha kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni kuidhurumu serikali inayokulipa kila mwezi na pia ni kwenda kinyume na taratibu za kiutumishi kwa kuwa motisha si lazima ila mtu hupewa anapoonyesha juhudi katika kazi,”amesema Mkurugenzi Sweya

Ameongeza kuwataka kutumia muda wanaokuwa ofisini kusoma sheria na miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali ili wawe na uelewa mpana wa mambo mbalimbali utakaowasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kuwa mambo yanabadilika kila siku.

“Nyie ni wasimamizi wa sheria katika maeneo yenu na mnamsaidia Mkurugenzi hivyo mbadilike kulingana na nyakati ili muweze kutimiza majukumu yenu vizuri na mjipange kwa kuwa mwaka wa fedha unaanza Julai tukaanze upya,”amesisitiza Mkurugenzi Sweya

Aidha amewataka kwenda kusimamia suala la ukusanyaji wa mapato na kufuatilia iwapo wanaojenga nyumba mpya wana vibali vya ujenzi kwa kuwa fedha hizo ndizo zinarudi kwa wananchi na kujenga madarasa, zahanati, mikopo na huduma mbalimbali za kijamii.

Aidha amewapongeza watumishi waliofanya vizuri na kuwasihi wengine kuiga mfano wa wenzao ikiwa ni pamoja na Halmashauri kufanya kazi kwa kushirikiana nao kwa kutatua changamoto walizoziwasilisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Utumishi na Utawala Ndg. Deogratious Nsanzugwanko amewataka watendaji kuzingatia sheria za utumishi wa umma na kanuni zake za mwaka 2022 ikiwemo wengi wao kubadilika kwa kutimiza wajibu wao.

“Kwanini tubembelezane watumishi hapa mnachelewa kazini katika vituo vyenu, kuondoka bila kuomba ruhusa na wengine kusafiri kabisa pamoja na kukiuka financial memorandum ya kukaa na fedha za serikali baada ya kuzikusanya,”amesema Ndg.Nsanzugwanko

Aidha amewakumbusha haki mbalimbali ambazo kama watumishi wanapaswa kuzipata ikiwemo kupanda cheo lakini wanapaswa kwanza kujaza Opras, likizo ya mwaka kila baada ya miezi 8 ya likizo ya awali, likizo ya ugonjwa na kuwasisitiza kuwa kupata kazi ni haki ya kila mtu pia watambue kufukuzwa kazi kupo.

Kikao kazi cha Watendaji wa Kata na Mitaa kimefanyika kwa lengo la kukumbusha masuala mbalimbali ya kiutendaji ambapo watendaji walijengewa uwezo na kilihudhuriwa pia na Wakuu wa Vitengo vya Sheria na Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • SHULE BORA yawapatia mafunzo ya tathmini Walimu 66 wa Kondoa Mji

    May 26, 2025
  • "Vitengo vya Mawasiliano Serikalini viimarishwe"

    May 24, 2025
  • Maafisa Habari hakikisheni wananchi wanapata habari sahihi

    May 23, 2025
  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa