• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Upimaji Viwanja Kuipandisha Thamani Bicha

Tarehe iliyowekwa: September 12th, 2018

Mtaa wa Bicha Halmashauri ya Mji Kondoa unatarajiwa kupanda thamani kutokana na zoezi la upimaji wa ardhi linalotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Hayo yalibainishwa na Bwana Juma Mustapha Afisa Mipango Miji wa Kampuni ya Makazi Solution wakati wa kikao cha maridhiano na wananchi wa mtaa huo kuhusu upimaji wa ardhi utakaofanyika katika mtaa huo.

“Ramani ya Mipango Miji imeshakamilika na imepita sehemu zote muhimu zoezi linaloanza sasa ni upimaji wa maeneo yenu na hii ni fursa kwenu kwani kwasasa mtajua kila eneo na matumizi yake.” Alisema Mustapha

Aliongeza kufafanua kuwa zoezi hilo la upimaji ni shirikishi ambapo litawashirikisha wananchi wenye maeneo na Kampuni ya upimaji ambao watafanya kazi kupitia Idara ya Ardhi ya Halmshauri ya Mji Kondoa.

Aidha aliwashauri wananchi wa Bicha kutouza maeneo yao kwasasa kwani kwa kufanya hivyo kunawapunguzia kipato kutokana na kuwa maeneo yao mengi hayajapimwa na hivyo kukosa thamani hivyo wawe na subira hadi maeneo yao yapimwe ambapo thamani itaongezeka na kuwapatia kipato zaidi.

“ Mradi huu unaenda kuwaneemesha wanaBicha na Kondoa kwa ujumla sababu kwa kupima eneo pia Halmshauri itapata mapato na Serikali kuu hivyo itaboresha huduma za kijamii Kondoa na nchi nzima pia nawe mwananchi utapata hati miliki ya eneo lako ambayo itakusaidia kupata mikopo katika taasis za kifedha na kuinua kipato chako na kupunguza migogoro ya ardhi.”Alisisitiza Mustapha

Kwa upande wake Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Bwana Anorld Mombeki aliwasihi wananchi kuiunga mkono kampuni hiyo na kutokuwa na wasiwasi nayo kwani wao kama wataalam wa ardhi wamejiridhisha utendaji kazi wao na uwepo wao kisheria na watafanya kazi wakiwa chini yao na kuwashauri wananchi wasioingia mikataba na kampuni kufika ofisi ya ardhi kupata ufafanuzi zaidi ili kuwajengea uelewa zaidi.

Hata hivyo mmoja ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo Mzee Seja aliishukuru kampuni kuja katika eneo lao kwa ajili ya kuongeza thamani maeneo yao na kuwahidi kuwaonyesha ushirikiano.

Mtaa wa Bicha ni moja ya Mitaa ya Halmashauri ya Mji Kondoa na upo katika barabara kuu ya Dodoma kuelekea Arusha ambapo Kampuni ya Mkazi Solution inatarajia kuanza zoezi la upimaji wa viwanja kwa kuingia mikataba na wananchi wenye maeneo na kugawana nao kwa kuwapatia asilimia 60 ya viwanja na wao kubakia na asilimia 40 ya viwanja ambapo viwanja 2700 vinatarajiwa kupimwa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa