• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Vikundi malezi wilaya ya Kondoa wapewa sungura kuboresha lishe endelevu

Tarehe iliyowekwa: May 30th, 2021

Na. Leah Joseph

Mratibu wa lishe endelevu Mkoa wa Dodoma Bw. Abdon Hamaro ameiasa jamii kuendelea kuwapatia watoto wenye umri chini ya miaka mitano,wajawazito na wanaonyonyesha chakula chenye virutubisho vyote ili kuepukana na tatizo la utapiamlo na udumavu ambalo limekuwa changamoto kwa jamii nyingi za Kitanzania.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara fupi ya kukagua mabanda ya kufugia sungura na kugawa sungura kwa vikundi malezi vilivyopo ndani ya Halmashauri ya Mji Kondoa hivi karibuni.

"Tumegawa sungura bure kwa kila wanakikundi lengo ni kuhakikisha kuwa tunaondoa tatizo la udumavu na lishe duni kwa watoto wanawake na vijana balehe hivyo basi mjitahidi kuwatunza vizuri ili waweze kukua na mwisho watumike kama inavyokusudiwa, "amesema Mratibu wa Lishe endelevu.

Ameendelea kusema kuwa Serikali ya Tanzania imeonesha jitihada kubwa kwenye masuala ya lishe kupitia mpango mkakati wa uratibu wa lishe kwenye sekta mtambuka hivyo basi mpango mkakati huo unaihakikishia Serikali kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na kuongeza idadi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa kula vyakula vyenye mchanganyiko wa kiwango kinachokubalika.

"Lishe endelevu itaisaidia Serikali kuongeza na kuboresha uwezo wa mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza mpango mkakati wa Taifa wa sekta mtambuka za lishe katika ngazi ya jamii lakini pia kurahisisha upatikanaji na utoaji wa huduma bora za lishe katika vituo vya afya pamoja na udhibiti wa usawa wa kijinsia katika mapato na matumizi ya rasilimali za nyumbani ili kuhakikisha upatikanaji wa vyakula mchanganyiko," amesisitiza Mratibu wa Lishe Bw. Abdon Hamaro.

Kwa upande wake mmoja wa wanufaika wa sungura kutoka kikundi malezi cha Chemchem  Bi Mwanate Hamis amewashukuru USAID kwa kuwapatia sungura hao na kuahidi kuwatunza na kuwatumia kama inavyokusudiwa.

"Tumefarijika sana kuona masuala ya lishe katika jamii yetu yanapewa kipaumbele na kuona umuhimu wa kuondoa tatizo la lishe duni unatekelezwa kwa vitendo na sisi tunaahidi kuwafuga kisasa ili waweze kuzalisha kwa wingi na kugawa kwa wengine ili jamii yote iweze kunufaika, "ameongeza Bi. Mwanate.

Ziara ya kugawa sungura kwa vikundi malezi ndani ya Halmashauri ya Mji Kondoa na Kondoa Vijijini imefanyika ikiwa ni muendelezo wa mpango mkakati unaotekelezwa na USAID kwa kushirikiana na wabia ukiwa na lengo la  kuondoa tatizo la udumavu na utapiamlo nchini huku Wilaya ya Kondoa ikiwa ni miongoni mwa wanufaika ndani ya Mkoa wa Dodoma ambapo ziara hiyo imeudhuliwa na Mratibu wa lishe Mkoa wa Dodoma, Afisa Kilimo Kondoa Mji, Kondoa Mji pamoja.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa