• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wafugaji Kondoa washauriwa kufuga kwa tija

Tarehe iliyowekwa: September 29th, 2021

Wafugaji Wilayani Kondoa wamewashauriwa kufuga kwa tija ili kuendana na soko la sasa na kuinuka kiuchumi.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Taifa Jeremiah Wambura wakati wa kikao cha pamoja na wafugaji wa Wilaya ya Kondoa kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni

“Niwaombe tuungane na kujenga mahusiano mazuri ili tuweze kufanikiwa katika ufugaji wetu lakini ni lazima tuje na mpango mkakati wa kuondoa kero zinazowakabili wafugaji ndani ya wilaya yetu na tuone namna ya kuvisaidia vijiji vyote vinavyokaa karibu na hifadhi kuhakikisha wote wapo salama bila kubugudhiwa ”amesema Wambura.

Ameendelea kuwaomba wafugaji kuwa mabalozi wazuri wa mazingira kwa kuhakikisha kuwa hawapeleki mifugo yao kwenye hifadhi  ili kuendelea kulinda mazingira lakini pia kuachana na migogoro isiyo na tija kwenye jamii bali wawe mfano wa kuigwa .

“Umefika wakati wa  kuachana na ufugaji wa zamani ambao mtu unakuwa na mifugo mingi ambayo haina faida zaidi ya kukuletea hasara hivyo basi tuzingatie hili na tukumbuke kwamba soko la sasa linataka nini, na kwamba bila kuwa na mifugo bora inayokidhi viwango tutakuwa tumeachwa katika soko la ushindani,”amesisitiza Wambura.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Kondoa Andrea Ng’wani akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya Mhe Khamis Mkanachi amemshukuru Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Taifa Jeremiah Wambura kwa kuweza kufika Kondoa na kuonana na wafugaji hao na kufanya nao kikao.

“Tunajua zipo changamoto nyingi zinazowakabili wafugaji wetu niseme tu tunazishughulikia japo hatuwezi kuzitatua kwa wakati mmoja  lakini kama wilaya tunatambua na kuheshimu uwepo wenu na mchango wenu kwa serikali yetu na kwa hilo nawapongeza sana,”amesisitiza Ng’wani.

Halikadhalika mmoja wa wafugaji Fatina Hussein amepata nafasi ya kutaka kujua ni kwanini voiwango vya chanjo vipo juu ikiwa kipato chao ni cha chini na alipatiwa ufafanuzi kuwa utaratibu huo ni  wa kawaida umewekwa na Serikali chini ya Wizara yenye dhamana hivyo kiwango wanachotozwa  ni halali kabisa.

Mkutano wa wafugaji na viongozi wa  Chama Cha Wafugaji umefanyika ukiwa na lengo la kujadili na kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji Wilaya ya Kondoa ambapo  wamepata nafasi ya kuchagua viongozi wao wa muda na umehudhuriwa na Viongozi wa Mkoa, Kanda, Wajumbe wa Kamati Tendaji pamoja na wafugaji kutoka Halmashauri zote za Wilaya ya Kondoa.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa