• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi Kondoa washauriwa kurasimisha maeneo kupata hati miliki

Tarehe iliyowekwa: May 9th, 2021

Wananchi wa Wilaya ya Kondoa wametakiwa kuhakikisha kuwa maeneo wanayomiliki yamerasimishwa na wanapata hati miliki ndani ya siku 90 kulingana na marekebisho ya sheria mpya ya ardhi namba nne ya mwaka 2020.

Kauli hiyo ameitoa  Afisa Tarafa ya Kondoa Mjini Ally Mbena wakati wa kikao cha kuhamasisha urasimishaji na upimaji wa ardhi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kondoa akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota hivi karibuni.

"Suala la urasimishaji na upimaji wa ardhi ni la kisheria hivyo nitoe rai kwa viongozi wa serikali za vijiji, mitaa na kata kuendelea kuhamasisha wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi kupimiwa maeneo yao na kupewa hati miliki, " amesema Mbena.

Aliendelea kusema kuwa wengi wanadhani kuwekewa alama za bikoni kwenye maeneo yao basi wamemaliza kazi lakini wanasahau kwamba hiyo haikupi sifa ya wewe kumiliki eneo hilo kisheria.

"Niwaombe viongozi wote kila mtu kwa nafasi yake tuende tukasimamie sheria tusiwe chanzo cha kukwamisha wananchi kupata hati miliki kwani kwa kufanya hivyo tunaikosesha Wilaya yetu mapato," amesisitiza Afisa Tarafa Mbena.

Hata hivyo aliongeza na kusema  kuwa ni wakati wa kuacha siasa na mijadara isiyo na malengo ni muda wa kuchapa kazi na kwamba serikali ya awamu ya sita iko macho hivyo kwa watendaji wote wanaofanya kazi kwa mazoea kuacha maramoja kwani mazoea yanapunguza ufanisi wa kazi lakini pia palipo na changamoto zisemwe ili zitatuliwe.

Kwa upande wake mwanasheria Halmashauri ya Mji Sued Shabani amewataka watu  kuelewa kwamba ardhi ni mali ya serikali na ndio maana inanunuliwa na kulipiwa kodi pamoja na kibali cha ujenzi.

"Mtu yeyote anapopata ardhi ahakikishe imepimwa na anapata hati miliki ndani ya siku 90 pia ni wajibu kulinda mipaka ya eneo lako ili kuepuka migogoro ya ardhi, "ameongeza mwanansheria.

Halikadhalika amewatahadharisha watu kuwa maeneo ya mijini yametengwa mahsusi kwa ajili ya mahitaji ya kudumu ambayo ni biashara na makazi na si vinginevyo hivyo kufanya shughuli za ufugaji na kilimo ni kosa kisheria, pia kabla hujajenga ni lazima uwe na kibali cha ujenzi.

"Kuna faida nyingi za kuwa na hati miliki kama vile kuongeza thamani ya eneo ambapo unaweza kukopesheka pia huondoa migogoro ya ardhi hivyo basi kila mtu awe balozi wa kuhamasisha wananchi ili waweze  kupata hati miliki na kulipia kodi ya ardhi ambayo itasaidia kuongeza mapato ya Halmshauri na Taifa kwa ujumla, "amesisitiza Mwanasheria  Shaban.

Kikao cha kuhamasisha urasimishaji na upimaji wa ardhi kimefanyika ikiwa ni agizo lililotolewa na Naibu Waziri wa ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Dkt Angela Mabula akiwataka watu kuwa na hati za umiliki wa maeneo yao ndani ya siku 90,ambapo kikao hicho kimehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji, Mwenyekiti wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani,Maafisa Ardhi kutoka Kondoa Mji na Kondoa Vijijini, Watumishi wa Halmashauri, Watendaji wa Kata na Mitaa, Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji pamoja na waandishi wa habari.


Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa