• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waratibu Elimu Kata na Walimu Wakuu wafundwa

Tarehe iliyowekwa: October 19th, 2018

Maafisa Elimu Kata na walimu wakuu wa shule za msingi katika Halmashauri ya Mji Kondoa wametakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma katika utendaji wa kazi zao za kila siku ili kuboresha elimu.

Hayo yalisemwa na Kaimu Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Mji Kondoa Mwalimu George Lukoa wakati wa kikao kazi kati ya watendaji wa Idara ya elimu msingi na viongozi hao wa elimu ngazi ya kata na shule katika ukumbi wa kituo cha walimu Iboni Kondoa mjini.

Alisema kuwa walimu wakuu ndio viongozi wa walimu shuleni hivyo wanapaswa kusoma saokolojia ya kila mwalimu jambo ambalo litawasaidia kupunguza migogoro makazini kwani itawarahisishia kujua jinsi ya kuenenda na kila mwalimu na kuwapa uhuru wa kuwasikiliza wanapowasilisha changamoto zao ili watatue kwa pamoja.

Aliongeza kwa kuwataka kuepuka kupokea rushwa za namna yoyote kutoka kwa walimu ili wawafichie madhaifu yao na wazazi ili kuwasaidia wanafunzi wakati wa mitihani jambo ambalo linadhalilisha taaluma yao na kuwashushia heshima kwa jamii lakini pia kuzalisha watoto wasio na maarifa yoyote.

“Twende tukafanye kazi kwa kushirikiana ili kujiandaa na mtihani wa darasa la nne tukajiandae vizuri na tuwaache watoto wakafanye mitihani wenyewe na tukatoe majaribio ya kutosha kwa kipindi kilichobakia, kuyasahihisha na kutoa matokeo kabla ya mtihani wa darasa la nne ili mtoto ajipime na kujirekebisha penye tatizo.”Alisisitiza Lukoa

Akiongea katika kikao hicho Mwalimu Egid Mhema kutoka Idara ya elimu aliwasihi walimu hao kusimamia nidhamu, malengo na majukumu waliyojiwekea ili kuongeza ufaulu pamoja na wastani wa ufaulu ili kushika nafasi nzuri kitaifa na inawezekana iwapo viongozi wote watashikamana kwa pamoja.

Akishukuru kwa niaba ya wenzie Afisa Elimu kata ya Kolo Mwalimu Magreth Stephen alishukuru viongozi wa wilaya kwa kuwakumbusha majukumu yao na kuwasihi maafisa elimu kata na walimu wakuu kufanya kazi kwa pamoja bila kujali kama shule ni ya serikali au binafsi ili kuongeza wastani wa ufaulu  ikiwa ni pamoja na kuendana na kasi ya awamu ya tano.

Kikao kazi cha viongozi wa elimu Idara ya elimu msingi, maafisa elimu kata na walimu wakuu kimefanyika ili kujiandaa na mtihani wa darasa la nne ikiwa ni pamoja na kukumbushana majukumu ya utendaji kazi na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha elimu ya msingi katika halmashauri ya mji Kondoa yenye jumla ya shule za msingi 29.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa