• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wasiohudhuria mkutano wa wananchi Unkuku kutozwa faini

Tarehe iliyowekwa: December 23rd, 2020

Wananchi wa Mtaa wa Unkuku kata ya Kilimani ambao hawakuhudhuria mkutano wa wananchi wa uhamasishaji wa ujenzi wa madarasa Shule ya sekondari Bicha wamepewa wiki moja kulipa faini ya shilingi elfu mbili ili iwe fundisho kwa wakati mwingine.

Hayo yamesemwa na Afisa Tarafa Kondoa Mjini Ally Mbena wakati wa mkutano wa wananchi wa mtaa huo uliofanyika katika uwanja wa ofisi ya Mtaa na kuhudhuriwa na wananchi wachache tofauti na idadi ya wakazi wa mtaa huo.

"Nimemuuliza Mwenyekiti mbona wananchi wachache leo tofauti na mkutano wa awali lakini kaniambia sababu ule ni mkutano wa masuala ya TASAF ndio maana wananchi walikuja wengi siyo sawa hii tusibague mikutano yatayozungumzwa  hapa yanahitaji maamuzi ya pamoja," amesema Mbena

Hata hivyo aliongeza kuwa jambo lililopo kwasasa ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Bicha hivyo ni wajibu wa wananchi wote kuchangia ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati kwani hadi sasa wapo nje ya wakati lengo ni kuhakikisha watoto wote waliofaulu wanaenda shuleni.

"Nawasihi sana ndugu zangu tuendelee pia kuwaandalia watoto wetu mahitaji muhimu ili shule zikifunguliwa waende shuleni kwani taarifa za ufaulu si za ghafla matokeo yamebandikwa wilayani lakini pia yatabandikwa ofisi ya Mtaa ili kila mtu aone mwanaye anaenda shule gani lakini nitumie fursa hii pia kuwakumbusha kuwaandikisha watoto wa awali na darasa la kwanza ili wapate haki yao ya msingi," amesisitiza Mbena.

Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Mwalimu Selina Fundi amesema kuwa ujenzi huo wa madarasa katika Shule ya Bicha umekuja kutokana na kuongezeka kwa ufaulu kwa mwaka huu ambapo jumla ya wanafunzi 279 wamechaguliwa kujiunga na shule hiyo hivyo mahitaji ni vyumba 6 na shuleni hapo kuna madarasa manne ndio maana umetokea upungufu wa vyumba viwili ambavyo tayari vimeanza kujengwa kwa kutumia mapato ya ndani.

"Maendeleo yanaletwa na sisi wananchi hivyo tukitoe kwa hali na mali kuhakikisha madarasa yanaisha lakini tutashirikiana na Halmashauri kujenga madarasa na pia tuna upungufu wa viti na meza 323 hivyo tutahitajika kujitoa pia kwa hilo na tumeshaanza upasuaji wa mbao ili kukabiliana na upungufu huo ili watoto wetu wasome katika mazingira mazuri,"amesema Mwalimu Selina.

Akitoa msimamo wa maazimio ya viongozi wa mtaa Kaimu Mtendaji wa kata ya Kilimani Merci Mmbasha amesema kila nguvu kazi katika mtaa huo itatoa shilingi elfu kumi na taarifa ya mapato na matumizi itasomwa katika mkutano wa mtaa ikiwa ni pamoja na kutoa majina ya watakaotoa na wasiotoa mchango.

Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ya wananchi na wataalam wa halmashauri katika kuhimiza ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo ulihudhuriwa pia na Afisa Maendeleo ya Jamii, Kaimu Afisa Mipango, Afisa Elimu Ufundi na Afisa Utamaduni na wananchi watatu walijitolea miti kwa ajili ya utengenezaji wa madawati.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa