• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Watendaji simamieni Mapato,miradi na utatuzi wa kero za wananchi"- Mkurugenzi Majaliwa

Tarehe iliyowekwa: March 26th, 2024

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa amewataka watendaji wa kata na mitaa kukuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato, miradi, kusikiliza na kutatua kero za wananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka kuzalisha kero mpya.

Ameyasema hayo wakati wa kikao chake na watendaji wa kata na mitaa ya Halmashauri ya Mji Kondoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

"Katika kipindi chote nitakachokuwepo Kondoa vipaumbele vyangu ni vitatu tu ambavyo nitavitumia kupima utendaji kazi wenu ambavyo mkifanya vizuri nyie ni sifa kwa Halmashauri na wala hamtagombana na mimi zaidi ya kuwa marafiki,"amesema Mkurugenzi Majaliwa

Amesema kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha watendaji wote wa kata na mitaa wanakusanya mapato ikiwa ji pamoja na kusimamia vyanzo vyote vya mapato katika maeneo yao ambapo hatamvumilia yeyote ambaye atasababisha upotevu wa mapato zaidi anategemea ushirikiano kwa kupatiwa taarifa za namna ya kuboresha njia za ukusanyaji wa mapato.

"Kama kuna mtu anakusanya fedha katika eneo lako mkague mara kwa mara na toa ushauri kwake kwa maandishi mkiboresha njia za ukusanyaji wa mapato ni rahisi kupata fedha za kurudisha kwenu na mkapata fedha za uendeshaji wa ofisi zenu na nitahakikisha nitasimamia mpate posho zenu,"amesisitiza Mkurugenzi Majaliwa

Ameongeza kwa kuwataka watendaji hao kuwa na taarifa zote muhimu za wafanyabiashara katika maeneo yao ikiwemo orodha yao na kufanya ukaguzi wa leseni zao na kuwa hatafurahishwa na Mtendaji ambaye hatakiwa na taarifa za makusanyo katika eneo lake.

Aidha amesema kipaumbele chake cha pili ni katika usimamizi wa miradi ambapo amewataka watendaji hao kuijua miradi yote katika maeneo yao na kuwaagiza watendaji wa kata kuhakikisha wanawawezesha watendaji wa mitaa kufika katika miradi yao.

"Tenga muda wa kutembelea miradi yako sintakuelewa endapo nitakuta mradi umesimama na hujatoa taarifa yoyote nijulisheni penye changamoto na tuwe na macho ya karibu si kwa miradi ambayo fedha zimeingia katika akaunti zenu bali kwa fedha pia zilizopelekwa moja kwa moja kwenye vituo kama shule na vituo vya afya,"amesema Mkurugenzi Majaliwa
Hata hivyo amewataka watendaji kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua bila kuangalia hali ya mtu na kuachana na tabia za kuwajibu vibaya wananchi na kutowafukuza ikiwa ni pamoja na kuwahudumia kwa moyo mmoja.
"Uongozi ni pamoja na kubeba na kupokea tukawasikilize wananchi na muwape majibu ya ukweli mwenye haki aipate na si kuwaambia nenda Halmashauri tusiwasumbue ikiwezekana piga simu omba ushauri tutakushauri ukiwa hukohuko na mkaweke kumbukumbu ya kero mnazozisikiliza na kuzitatua kwenye daftari la malalamiko,"ameshauri Mkurugenzi Majaliwa
Kikao cha watendaji wa kata na mitaa na Mkurugenzi kimefanyika ikiwa ni mwendelezo wa vikao vyake vya kukutana na watumishi mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza changamoto zao mara baada ya kuhamia katika Halmashauri ya Mji Kondoa kutoka Halmashauri ya jiji la Tanga.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Baraza la Madiwani lajivunia mafanikio kipindi cha miaka mitano

    April 30, 2025
  • Baraza la kazi robo ya tatu lafanyika Kondoa Mji Ushirikiano ukisisitizwa

    April 29, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa